Monday 17 December 2018

Niruhusu Nikuite Baraddhuli


Kama kuku kwao mtama, chambo chako kikanasa,
Na kwa mkunjufu mtima, ‘kamchagua mkongwe hasa,
Matumaini yazama, vijana kwenye anasa
‘Kiniruhusu raisi, ‘takuita baradhuli

Kwa mapana na marefu, ukamteua Awori,
Nchi yetu tukufu, ‘mebaki la wenye gari,
Wakupa sifa sufufu, mwenye njaa ale mori,
‘Kiniruhusu raisi, ‘takuita baradhuli


Ulisimama jukwaani, ukanena wazi wazi,
Kama kundule kwa nyani, azma ya kijana wizi
Wamo wenye mvi vichwani, ila linavuja zizi
‘Kiniruhusu raisi, ‘takuita baradhuli



No comments:

Post a Comment